1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi. Merkel ziarani India.

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7B4

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza siku ya pili ya ziara yake ya kiserikali nchini India kwa kukutana na wasanii na wasomi wengine. Amekuwa pia akizungumza na vijana wenye ujuzi katika kituo cha utamaduni wa Ujerumani , Goethe Institute, mjini New Delhi. Merkel baadaye atakwenda katika mji wa kibiashara na fedha wa Mumbai nchini India. Jana Jumanne kansela alikutana na waziri mkuu wa India Manmohan Singh. Wamekubaliana kujaribu kuongeza maradufu biashara kati ya nchi hizo kila mwaka hadi Euro bilioni 20 katika muda wa miaka mitano ijayo.