NEW DELHI: Msimu wa masika wasababisha mafuriko India
23 Juni 2007Matangazo
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini India yameua si chini ya watu 39.Katika jimbo la kusini la Andhra Pradesh,hadi watu 35 walifariki katika mafuriko ya ghafula katika kipindi cha saa 24.Si chini ya wakazi 200,000 wamehamishwa maeneo mengine.Vile vile watu 4 walifariki katika jimbo la Kerala.Msimu wa masika umesababisha hasara kubwa na umevuruga usafiri wa matreni na magari.