NEW DELHI: Pakistan na India zakubali mkataba wa kupiga vita ugaidi
16 Novemba 2006Matangazo
India na Pakistan zimekubaliana kuhusu mkataba unaoeleza njia za kushirikiana kupiga vita ugaidi.Pande hizo mbili zimekutana mjini New Delhi kwa mazungumzo ya amani ya siku mbili.Hayo ni mazungumzo ya kwanza ya amani kufanywa kati ya nchi hizo,tangu kutokea mashambulio ya kigaidi ya mwezi Julai katika treni mbali mbali mjini Mumbai na kuua takriban watu 200.Kufuatia mashambulio hayo,serikali ya India ilisitisha majadiliano yote na ikatuhumu kuwa makundi yalioungwa mkono na serikali ya Pakistan yalihusika na mashambulio hayo.Nchi hizo mbili katika mkutano wa New Delhi zimekubali pia kubadilishana habari za upelelezi ili kupunguza hatari ya kutokea mpambano wa kinuklia kwa makosa.