1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI-Raia wa Kashmir wa India na Pakistan watembeleana

7 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPY

Basi lililokuwa limewachuka abiria kutoka eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India,limevuka mpaka na kuingia katika eneo la Kashmir la Pakistan,katika safari ya kwanza ya usafiri wa basi kuvuka mpaka huo,tangu eneo la Kasmir lilipogawanyika kufuatia vita kiasi cha miaka 60 iliyopita.

Baadae raia 19 wa India walivuka mpaka na kuingia eneo la Pakistan na kupanda mabasi ya Pakistani wakiwa wanaelekea katika kituo cha uhamiaji na baadae wakaendelea na safari yao,ikiwa ni saa chache tu baada ya Wakashmir wa Pakistan,nao kuvuka na kuingia India wakiwa wanaelekea katika mji mkuu wa Kashmir wa Srinagar.

Huduma mpya ya usafri wa mabasi kati ya Srinagar na Muzaffarabad,mji mkuu wa Kashmir ya Pakistan,ni mwanzo wa hatua muhimu kuelekea mchakato baina ya India na Pakistan.

Mataifa hayo mawili jirani ambayo yote na nguvu za nyuklia,yalikaribia kupigana vita kamili mwaka 2002.