1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi. Rais wa Pakistan azuru India.

17 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMI

Rais wa Pakistan Bwana Pervez Musharaf ameanza ziara yake muhimu nchini India. Ziara ya Bwana Musharaf, ya kwanza katika muda wa miaka minne, itajumuisha pamoja na kukutana na waziri mkuu wa India , Bwana Manmohan Singh na kuangalia mchezo wa kriket kati ya India na nchi yake.

Viongozi hao wawili watajadili masuala nyeti kama ya eneo la Kashmir lililogawanywa, sehemu ambayo nchi hizo jirani zenye silaha za kinuklia zilipigana vita mara mbili na kukaribia kupigana mara ya tatu. Viongozi hao pia watangalia njia za kuimarisha zaidi uhusiano wao ambao unazidi kuwa bora.

Ghasia katika jimbo la Kashmir ziliendelea jana wakati majeshi ya India yalipowauwa wapiganaji wawili wa chini kwa chini wa kundi la Hizboul Mujahedeen.

Siku moja kabla , wanajeshi waliwapiga risasi na kuwaua wapiganaji wanne wa kundi tofauti la wapiganaji ambalo linapinga utawala wa India katika sehemu ya Kashmir.