1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi. Uchumi wa India juu.

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCj2

Ukuaji wa uchumi nchini India unatarajiwa kuwa wa kwanza katika mataifa ya bara la Asia mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya benki kuu ya dunia, ambayo inaonesha uchumi wa nchi hiyo utakua kwa asilimia 8.7. Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu bilioni 1.2 katika mataifa yanayoendelea wataingia katika tabaka la kati duniani ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni ongezeko kutoka watu milioni 400 hivi sasa.