1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New Delhi. Viongozi wa India na Pakistan wataka ushirikiano zaidi katika jimbo linalogombaniwa la Kashmir.

18 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFLt

Viongozi wa India na Pakistan wamesema kuwa hatua za kuleta amani kati ya nchi hizo mbili haziwezi kurudi nyuma. Katika hatua muhimu mwishoni mwa ziara yake mjini New Delhi, rais wa Pakistan Bwana Perves Musharaf alijiunga na waziri mkuu wa India Manmohan Singh katika kutangaza kuwa watafanyakazi kuelekea kuwa na mpaka usio na matatizo katika Kashmir.

Wanapanga kufungua vituo vya kukutania katika eneo hilo linalogombaniwa kwa ajili ya familia zilizotengana na kuimarisha biashara, misafara na ushirikiano katika mpaka. Akisoma taarifa yao ya pamoja Bwana singh amesema kuwa pande hizo mbili zinafahamu haja kubwa wa watu wa nchi hizo mbili ya kuwa na amani ya kudumu.

Hata hivyo , hakuna hatua iliyopigwa kuelekea kupatikana suluhisho la kudumu kuhusu Kashmir wakati wa ziara ya siku tatu ya Jenerali Musharaf.