1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI:Kansela Angela Merkel amewasili nchini India

30 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BL

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara ya siku nne nchini India.

Bibi Merkel amepokelewa kwenye uwanja wa ndege wa New Delhi kwa heshima za kijeshi na waziri mkuu wa India Manmohan Singh.

Ziara ya kiongozi huyo wa Ujerumani inalenga kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na ushirikiano katika sekta ya sayansi na siasa.

Kansela Merkel ameandamana na wanauchumi wa Ujerumani.

Mbali na masuala ya ushirikiano wa kiuchumi,kisayansi na kisiasa mada nyingine katika mazungumzo ya viongozi wa Ujerumani na India zinahusu misaada ya maendeleo ya Ujerumani, hifadhi ya hali hewa na mchango wa mwanamke katika jamii.

Akiitemebela sehemu ya makumbusho ya Mahatma Gandhi kansela Angela Merkel amemsifu kiongozi huyo wa vuguvugu la uhuru wa India kuwa ni mfano wa kiongozi wa taifa anaestahiki kuigizwa.