NEW DELHI:Mvua kubwa zimesababisha hasara India na Pakistan
9 Agosti 2006Matangazo
Kiasi ya watu 200 wamefariki katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua za masika,magharibi na kusini mwa India.Mafuriko hayo yameporomosha nyumba na kiasi ya watu 650,000 wamelazimika kukimbilia maeneo ya juu.Jeshi linatumia helikopta na boti kusaidia maelfu ya watu walionasa.Nchini Pakistan vile vile,mafuriko ya ghafula yaliyosababishwa na mvua kubwa yameua zaidi ya watu 140 katika eneo la kaskazini-magharibi.Mafuriko hayo yamesababisha pia hasara kubwa ya mali na vijiji mia kadhaa vimezama chini ya maji.