1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW DELHI:Ujerumani na India kuongeza nguvu shughuli zao za kibiashara

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BF

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema nchi yake na India zinampango wa kuongezea nguvu shughuli zao za kibiashara kwa euro billioni 20 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Kansela Ameyasema hayo mbele ya waandioshi wa habari mjini New Delhi baada ya kukutana na waziri mkuu wa India Manmohan Sighn.Aidha Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema nyanja nyingine za ushirikiano wa kibiashara zitakazoimarishwa ni upande wa sayansi na juhudi za kupambana na ongezeko la Ujoto duniani.Kwa upande wmingine waziri mkuu wa India ameitaja mipango hiyo kuwa hatua mpya katika mahusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Viongozi hao wawili wametia saini mikataba saba yenye lengo la kuimarisha mkakati wa kibishara kati ya nchi hizo mbili.Kansela Merkel leo atakuwa mjini Mumbai kuhutubia baraza la ushirikiano wa kiuchumi la Ujerumani na India.