NEW YORK : Baraza la usalama lajadili azimio dhidi ya Korea Kazkazini
7 Julai 2006Matangazo
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeanza tena mjadala wa azimio la pamoja kuyalaani majaribio ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Korea Kazkazini.
China na Urusi zinapinga vikwazo vya kiuchumi dhidi ya serikali ya Pyongyang, zikipendekeza kuanza tena kwa mazungumzo ya mataifa sita kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea Kazkazini.
Korea Kazkazini imeapa kufanya majaribio zaidi na kutishia kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya taifa lolote litakalojaribu kuizuia.
Nchi hiyo ilifanya majaribio saba ya makombora juzi Jumatano. Jaribio moja la kombora aina ya Taepodong 2 linaloaminiwa linaweza kufika jimbo la Alaska nchini Marekani, halikufaulu.