1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Baraza la Usalama lajadili Burma

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kufikia makubaliano kamili juu ya taarifa yenye kushutumu hatua ya serikali ya Myanmar kuvunja kwa kutumia nguvu maandamano ya kudai demokrasia.

Wanadiplomasia wanasema mabalozi inabidi wawasiliane na serikali zao kabla ya kuidhinishwa rasmi kwa waraka huo. Kipengele kigumu ni juu ya maneno ya kutumia katika suala la kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa na mahabusu.Taarifa hiyo ni hatua ya kwanza kuchukuliwa na Baraza la Usalama kwa Myanmar.

Utawala wa kijeshi wa Myanmar umekuwa chini ya shinikizo kali la kimataifa kwa kuvunja kwa nguvu maandamano ya maelfu ya watatezi wa demokrasia waliokuwa wakiongozwa na watawa Wakibuda hapo mwezi wa Septemba na mapema mwezi wa Oktoba.

Takriban watu 13 wameuwawa katika ghasia hizo.