NEW YORK: Korea Kaskazini kuonywa kuhusu jaribio la kinuklia
6 Oktoba 2006Matangazo
Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekubaliana na hati iliyopendekezwa na Japan.Mswada huo unaionya Korea ya Kaskazini kuwa pindi itafanya jaribio lake la kinuklia, itakabiliwa na matokeo ambayo hayakutajwa.Balozi wa Japan katika Umoja wa Mataifa,Kenzo Oshima amesema,mswada huo unapelekwa kwa serikali za wanachama 15 wa baraza hilo,pindi unahitaji kufanyiwa mabadilisho,lakini inaaminiwa kuwa hati hiyo itaidhinishwa baadae leo Ijumaa.Wakati huo huo Urussi imesema inawasiliana na Korea ya Kaskazini moja kwa moja,kujaribu kuizuia kufanya jeribio lake la silaha ya kinuklia.Siku ya Jumanne,Korea ya Kaskazini ilitangaza kuwa itajaribu silaha yake ya kinuklia,lakini tarehe yenyewe haikutajwa.