NEW YORK: Korea Kaskazini labda ina silaha za kinyuklia
9 Mei 2005Matangazo
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Kinyuklia la Umoja wa Mataifa,Mohamed ElBaradei amesema Korea Kaskazini huenda ikawa ina silaha za kinyuklia.Katika mahojiano yake na televisheni ya CNN,ElBaradei amesema,serikali ya Pyongyang ina madini ya plutonium na miundo mbinu ya kiviwanda inayohitajiwa kutengeneza silaha tano hadi sita za kinyuklia.