1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Korea ya kaskazini kuwekewa vikwazo.

14 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD35

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limekubaliana kuhusu maandishi ya azimio litakaloweka vikwazo dhidi ya Korea ya kaskazini kwa kufanya jaribio la silaha za kinuklia , na kura ya mwisho itafanyika leo Jumamosi.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa John Bolton , ametangaza azimio hilo katika kikao cha faragha cha baraza jana Ijumaa.

Muswada huo mpya haujumuishi tena vikwazo vya silaha lakini unasisitiza upekuzi wa anga na bahari katika mizigo inayoingia na kutoka katika taifa hilo la kikomunst.

Japan imekwisha anza utekelezaji wa hatua hizo dhidi ya Pyongyang, ikiwa ni pamoja na marufuku dhidi ya uagizaji kitu chochote kutoka Korea ya kaskazini na kuinyima nchi hiyo , meli zake kufunga gati katika bandari za Japan.

Wakati huo huo , ndege zenye vifaa maalum za Marekani zimegundua ushahidi wa mwanzo wa uwezekano wa miale ya kinuklia katika eneo la Korea, ambayo inaweza kuthibitisha madai ya Korea ya kaskazini kuwa imefanya jaribio la bomu la Atomic.