1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Korea ya kaskazini yatakiwa kuacha kufanya majaribio yake ya kinuklia.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5C

Wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wamepiga kura kwa kauli moja kuidhinisha taarifa ya pamoja inayoitaka Korea ya kaskazini kuacha kufanya majaribio yake ya silaha za kinuklia.

Maafisa wa Japan wamesema kuwa wanaamini Korea ya kaskazini huenda ikafanya majaribio hayo mwishoni mwa juma hili.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa anasema kuwa nchi yake inataka kupata mkakati makini kutokana na kile alichokieleza kuwa na hatua ya kuijaribu jumuiya ya kimataifa.

Korea ya kaskazini imetangaza mipango yake ya majaribio ya kinuklia mapema wiki hii, ikisema kuwa ni muhimu kwa kuzuwia matumizi ya mabavu ya Marekani, kiuchumi na kijeshi.