1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Marekani yashutumu Umoja wa Mataifa kwa msaada wa kifedha kwa Korea Kaskazini.

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZR

Marekani imelishutumu Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa madai kwamba huenda mamilioni ya fedha za msaada zilitolewa kwa serikali ya Korea Kaskazini ya Kim Jong Il.

Naibu balozi wa Marekani wa Umoja wa Mataifa, Mark Wallace, amelishutumu shirika hilo kwa kukiuka kwa muda mrefu kanuni za Umoja huo liliporuhusu fedha kupelekwa katika taifa hilo la Kikomunisti.

Mark Wallace amesema kuna wasiwasi huenda fedha hizo zimetumika kugharamia mradi wa silaha za kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Wakuu wa Umoja wa Mataifa wamesema watafanya uchunguzi kamili kuhusu suala hilo na kwamba watumishi wa Umoja huo walioko Korea Kaskazini watakuwa wakilipwa mishahara yao kwa sarafu ya taifa hilo.