1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK. Mjumbe wa umoja wa mataifa Korea Kazkazini aondolewa.

21 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFL2

Mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Korea Kazkazini, Maurice Strong, ametimuliwa na nafasi yake ikachukuliwa na Inga-Britt Ahlenius wa Sweden. Strong ameondolewa kutoka wadhifa wake kwa uhusiano wake na mtu anayetuhumiwa kuhusika katika kashfa ya chakula kwa mafuta nchini Irak.

Mfanyabiashara huyo wa Canada, amekiri alikuwa na uhusiano wa kibiashara na Park Tongsun wa Korea Kusini, anayekabiliwa na mashtaka ya kuwapa hongo maafisa wa umoja wa mataifa kwa niaba ya serikali ya rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein. Strong ameziongoza juhudi za mazungumzo ya kimataifa kuhusu mpango wa nuklia wa Pyongyang.