1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Mradi wa kinuklia wa Korea Kaskazini wajadiliwa

7 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF69

Maafisa wa Marekani na Korea ya Kaskazini wamekutana mjini New York kuujadili mradi wa kinuklia wa serikali ya Pyongyang.Hii ni mara ya pili kwa maafisa wa pande hizo mbili kukutana katika kipindi kischopindukia hata mwezi mmoja.Majadiliano ya madola 6 kuhusu mradi wa kinuklia wa Korea ya Kaskazini yamekwama tangu mwezi wa Juni mwaka jana,baada ya nchi hiyo kuondoka mkutanoni.Serikali 6 zinazojishughulisha na majadiliano hayo ni China,Japani,Korea zote mbili,Russia na Marekani.