NEW YORK. Shirika la afya duniani lasema baadhi sampuli za virusi hazijulikani ziliko.
15 Aprili 2005Matangazo
Shirika la afya duniani linasema mahabara mengi kati ya 3,700 zilizopokea sampuli za virusi hatari wanaosababisha homa kali ya Asian, zimeziharibu sampuli hizo. hata hivyo mwanasayansi mkuu wa shirika hilo anasema kuna ripoti ya kutia hofu kwamba baadhi ya sampuli za virusi hao hazikuorodheshwa na hazijulikani ziliko. Klaus Stohr alisema mahabara mbili nchini Mexico na Lebanon hazikuorodheshwa na zilipokea sampuli hizo.