1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Uamuzi usiptishwe kwa haraka kuhusu Korea Kaskazini

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3N

Urussi na China zinataka muda zaidi kushauriana juu ya mswada unaohusika na Korea ya Kaskazini. Mabalozi wa nchi hizo mbili katika Umoja wa Mataifa mjini New York,wametoa mwito kwa Marekani kujadiliana zaidi juu ya mswada uliopendekezwa na serikali ya Marekani.Baada ya Korea ya Kaskazini kutangaza kuwa imefanya jeribio la kinuklia, Marekani imetoa mwito wa kuchukua hatua kali za vikwazo dhidi ya Pyongyang.Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,John Bolton amewasilisha kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mswada uliofanyiwa marekebisho akitumaini kuwa utaidhinishwa leo hii.Urussi imesema,jaribio la kinuklia la Korea ya Kaskazini lapaswa kuchukuliwa hatua kali,lakini uamuzi huo upitishwe kwa utulivu.China nayo imesema,azma ya Umoja wa Mataifa isiwe ni kutoa adhabu tu.