NEW YORK : Umoja wa Mataifa waionya Korea Kaskazini
7 Oktoba 2006Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana kwa kauli moja limeitaka Korea Kaskazini kutelekeza mpango wake wa jaribio la kwanza la bomu la nuklea.
Japani imesema Korea Kaskazini yumkini ikafanya jaribio hilo mwishoni mwa juma hili ikiwa ni siku tatu baada ya kutangaza nia yake hiyo.Baraza la Usalama limeonya kwamba iwapo Korea Kaskazini itafanya jaribio hilo itakabiliwa na madhara ambayo hayakutajwa na imetaka badala yake nchi hiyo irudi kwenye mazungumzo yanayojumuisha pande sita ambayo Korea Kaskazini ilijitowa mwaka mmoja uliopita.
Marekani na Korea Kusini zote ziliwahi kuonya kwamba haziwezi kuvumilia kuwepo kwa taifa la Korea Kaskazini lenye kumiliki silaha za nuklea.Russia na China zimeitaka Korea Kaskazini kujizuwiya kuchukuwa hatua hiyo.
Duru za China zinasema Korea Kaskazini inapanga kufanya jaribio hilo la bomu la nuklea mita 200 chini kwenye mgodi wa zamani wa makaa ya mawe.