NEW-YORK:''Gorge.W.Bush ni Ibilisi ''asema Hugo Chavez
21 Septemba 2006Matangazo
Rais wa Venezuela Hugo Chavez ameishutumu Marekani kwa kuligeuza baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuwa chombo kisichokuwa na maana kwa kuzipokonya nguvu nchi ndogo.
Rais Chavez akihutubia katika mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa hapo jana alifika umbali wa kumuita rais Gorge Bush ibilisi. Rais Chavez pia amesema Bush ni dikteta wa dunia ambaye anayehitaji tiba ya ugonjwa wa akili.Hotuba yake hiyo ilipigiwa makofi na baadhi ya wajumbe waliokuwa kwenye mkutano huo wa Umoja wa mataifa.
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice hakufurahishwa na hotuba hiyo akisema kwamba hawezi kuyatukuza maoni ya rais Chavez kwa kutoa maoni yake.