1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Uamuzi wa India-Pakistan wakaribishwa

7 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlJ
Jumuiya ya Kimataifa imeukaribisha uamuzi wa India na Pakistan wa kuanza tena mazungumzo miaka miwili baada ya nchi hizo nusura kuingia katika vita vyao vya nne. Mazungumzo hayo rasmi yaliopangwa kufanyika mwezi wa Februari yatajadili mizozo ukiwemo ule wa Kashmir.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema ufumbuzi wa mgogoro huo utalinufaisha eneo zima la Kusini mwa Asia wakati Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Romano Prodi ameuita uamuzi huo wa kurudi katika meza ya mazungumzo kuwa ni thibitisho la kujizatiti kwa nchi hizo mbili kutatuwa mizozo kati ya nchi hizo Ujerumani imesema inataraji mazungumzo hayo yataweza kurudisha uhusiano wa kudumu baina ya nchi hizo jirani.