NEWYORK:Japan yawasilisha azimio juu ya Korea kaskazini
9 Julai 2006Japan imewasilisha mbele ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa mjini Newyork Marekani,azimio litakaloweza kuiweka vikwazo Korea Kaskazini kufuatia majaribio ya makombora yake hivi karibuni.
Mabalozi wa Japan,Ufaransa na Marekani wamesema azimio hilo litapigiwa kura jumatatu ijayo.Awali Japan ilikuwa inatia msukumo kura hiyo ipigwe jana jumamosi lakini balozi wa China katika Umoja wa mataifa Wang Guangya akaonya kwamba hakutakuwa na mshikamano.
Azimio hilo limekuja baada ya Korea Kaskazini kuanzisha majaribio ya makombora yake kiasi saba siku ya Jumatano ikiwa ni pamoja na lile lenye masafa marefu ambalo baadhi ya wataalamu wanasema huenda likafika hadi Alaska Marekani.
Wakati huo huo mtaalamu wa Marekani wa kuharibu makombora amekwisha wasili kwenye ngome ya kijeshi ya Marekani ya Yokosuka, Tokyo.