Timu ya taifa ya kandanda ya Rwanda haitokuwa miongoni mwa timu zitakazoshiriki mashindano yajayo ya kuwania ubingwa wa mataifa barani Afrika AFCON baada ya kupata kichapo cha 2-0 nyumbani kwao Kigali mikononi mwa Msumbiji hapo Jumapili. Christopher Karenzi amekusanya yaliyojiri michezoni nchini humo mwishoni mwa wiki iliyokwisha.