Guterres: Njaa inahatarisha amani duniani
14 Februari 2024Guterres amewaambia wajumbe kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa ngazi ya juu kuwa majanga ya mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri uzalishaji wa chakula na kwamba njaa inachochea machafuko.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama lizikabili athari zinazotokana na upungufu wa chakula pamoja na zile zinazosababishwa na ongezeko la joto.
soma pia:Mabadiliko ya tabia nchi ni kiticho kikubwa cha usalama wa chakula
Mkuu wa kitengo cha maswala ya hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa Simon Stiell, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mabadiliko ya tabia nchiyanasababisha ukosefu wa uhakika wa upatikanaji wa chakula na pia amesema hali hiyo inachochea migogoro. Ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kupunguza nishati zinazoharibu mazingira.