Suala la utasa au ugumba kwa jumla ni kero kubwa miongoni mwa wanandoa hasa wanawake. Kwa bahati mbaya jambo hilo halijatiliwa maanani na mamlaka za afya katika nchi nyingi za Afrika wakati wanapozingatia suala jumuishi la afya ya uzazi. Hali hii imewaacha wanandoa wengi katika unyanyapaa kwani ni wale tu walio na nafasi bora za kifedha ndiyo hufanya kila juhudi kupata huduma za uzazi saidizi.