1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Norway kuchukua jukumu la ulinzi wa anga wa Poland

3 Desemba 2024

Norway itachukuwa majukumu ya kulinda usalama wa anga ya uwanja wa ndege wa Poland wa Rzeszow chini ya mamlaka ya Jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4ngRK
 F-35
Ndege za kivita chapa F-35Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Nchi hiyo itapeleka kikosi chake cha wanajeshi 100, mifumo ya ulinzi wa anga pamoja na ndege za kivita chapa F-35 kusimamia ulinzi.

Hayo yametangazwa na waziri wa ulinzi wa Norway Bjorn Arild Gram, ambaye pia amefafanuwa kwamba uwanja huo wa ndege wa Poland ni muhimu kwa usafirishaji wa vifaa vya kijeshi na  pia shughuli za usafirishaji wa dharura wa wanaohitaji huduma za matibabu, zinazosimamiwa na Norway.

Kwa mujibu wa Norway mifumo ya ulinzi, wanajeshi na ndege za kivita zitapelekwa katika kipindi cha siku kadhaa zijazo na ujumbe huo wa Norway utaendesha shughuli zake hadi msimu wa Pasaka.