1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu-finali ya champions League

23 Aprili 2008

Baada ya jana Liverpool kuondoka sare bao 1:1 na Chelsea ,leo ni zamu ya FC Barcelona na Manchester United.

https://p.dw.com/p/DnRP

Baada ya jana timu 2 za Uingereza-Chelsea na Arsenal kutoka suluhu bao 1:1 katika changamoto za nusu-finali za champions League-kombe löa klabu bingwa barani Ulaya, leo ni zamu ya Manchester United na FC Barcelona kunyan'ganyia nafasi ya pili ya finali ya kombe hilo.

Silvio Berlusconi asikitika kubidi kujiuzulu kama rais wa AC Milan baada ya kuchaguliwa tena waziri mkuu wa Itali na wanariadha wa Ethiopia wanadai watatamba katika mashindano ya wiki ijayo ya ubingwa wa riadha barani Afrika.

►◄

Macho ya mashabiki wa dimba wa Uingereza yanakodolewa jioni hii katika uwanja wa Nou Camp ambako Manchester inarudi kujikumbusha mojawapo ya ushindi wake mkubwa katika historia ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.Mahasimu wao huko ni wenyeji FCBarcelona ambayo katika mapambano 2 yaliopita ya Ligi nyumbani walimudu sare tu ya 0:0.Pia jogoo wao Ronaldinho anataka kuwaacha mkono na kuhamia Ligi nyengine msimu ujao.

Manchester inaendelea kutamba katika Premier League-ligi ya Uingereza na ilitamba tena mwishoni mwa wiki.

Mpambano huu wa leo huenda ukaamua hatima ya kocha wa Barcelona-mholanzi Frank Rijkaard,kwani ikiwa Barcelona itashindwa kukata tiketi ya finali ,basi huenda akatimuliwa.

Sir Alex Ferguson, hana wasi wasi ,kwani kiti chake ni imara na hakuna kwa sasa msumeno wowote wa kuweza kukikata.

Endapo Liverpool iliomudu jana suluhu na Chelsea ikipigwa kumbo mwishoe nje ya finali ya kombe hili mwezi ujao, kuna fununi kocha wao Benetiz ataiaga Liverpool na kuhamia Spain ,kuiongoza Barcelona.

Kufuatia nusu-finali ya kwanza hapo jana, Chelsea ina matumaini ya kucheza kwa mara ya kwanza finali ya kombe la klabu bingwa.Kwa kweli, Liverpool ilijichimbia kaburi yenyewe pale John Arne alipoutia kichwa mpira maridadi ajabu langoni mwake.

Baada ya kupewa zawadi hiyo ya bao dakika ya mwisho ya mchezo ,Chelsea ya akina Didier Drogba na Michael Ballack inatumai sasa kuonana finali ama na Manchester au na Barcelona.Mradi tu itambe nyumbani katika marudio .Liverpool ilitangulia kwa bao la Dirk Kuyt mnamo dakika ya 43 ya mchezo .Lakini zikisalia sekunde tu firimbi ya mwisho kulia, John Arne alilifumania lango lake mwenyewe na kuwaokoa Chelsea .

Baada ya wiki moja, Chelsea ina nafasi ya kuizika kabisa Liverpool katika changamoto yao ya 3 ya nusu-finali mnamo muda wa miaka 4 na kukata tiketi ya finali mjini Moscow hapo Mei 21.

Tajiri anaemiliki AC Milan,mabingwa wa ulaya msimu uliopita, Silvio Berlusconi,amesema anahuzunishwa kubidi kujiuzulu kama rais wa AC Milan pale atakaposhika wadhifa wa waziri mkuu kwa mara ya 3 nchini Itali.

Berlusconi, mwenye umri wa miaka 71 yamkini atamuachia usukani makamo-rais wa sasa wa klabu hiyo Adriano Galliani ambae alitumika katika cheo hicho pale Berlusconi alipokuwa waziri mkuu 2001-2006.

RIADHA:

Ethiopia inalenga kuzoa medali zote katika mbio za masafa marefu wakati wa mashindano ya wiki ijayo ya ubingwa wa riadha wa Afrika mjini Addis Ababa.

Zaidi ya wanariadha 2,000 kutoka nchi 43 mbali mbali za Afrika watashiriki kuanzia April 30 hadi mei 4.Mashindano haya yatawanoa mabingwa wa Afrika -wake kwa waume-kwa michezo ijayo ya olimpik mjini Beijing hapo August.

Bingwa wa Olimpik na wa rekodi ya dunia Kenenisa Bekele ataongoza kikosi cha waethiopia katika zahama za mbio za mita 10.000 wakati timu yao ya mita 5000 itaongozwa na tariku Bekele.Bingwa wa dunia wanawake Tirunesh Dibaba atatamba katika mita 10.000 akimuachia Meseret defar usukani wa mita 5000.

Mashindano ya riadha ya ubingwa wa Afrika hufanyika kila baada ya miaka 2.