1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama amteuwa waziri mpya wa afya

Miraji Othman1 Machi 2009

Obama amteuwa waziri mpya wa afya

https://p.dw.com/p/H3ci

Washington:


Rais Barack Obama wa Marekani amemteuwa gavana wa mkoa wa Kansas, Bibi Kathleen Sebelius, kuwa waziri wa afya wa nchi hiyo. Bibi huyo, mwenye umri wa miaka 60 kutokea Chama cha Democratic, ameukubali uteuzi huo. Uteuzi huo utatangazwa rasmi kesho. Mtu ambaye rais Obama mwanzo alipendelea akamate wadhifa huo, Tom Daschle, aliacha kuuwania wadhifa huo mwanzoni mwa mwezi uliopita pale ilipojulikana kwamba ana matatizo na ofisi ya kodi. Rais Obama ameliweka suala la kuufanyia mageuzi mfumo wa afya wa Marekani kuwa ni muhimu katika siasa yake. Hivi sasa karibu Wamarekani milioni 50 hawana bima za afya.