1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ocampos aiwezesha Sevilla kutinga nusu fainali

Deo Kaji Makomba
12 Agosti 2020

Mshambuliaji Lucas Ocampos ameiwezesha timu yake ya Sevilla kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi Ulaya, Europa league, baada ya kuifungia timu yake bao pekee la ushindi katika dakika za lala salama.

https://p.dw.com/p/3gr2q

Fußball Freundschaftsspiel | Deutschland vs Argentinien
Picha: Reuters/L. Kuegeler

Sevilla ilitawala mapumziko ya mchezo wakati Wolves inavyozidi kuchoka katika mchezo wake wa 59 wa msimu mrefu. Goli lilionekana haliwezi kuepukika na Lucas Ocampos akaukwamisha mpira huo kwa kichwa kunako dakika ya 88 na kuiwezesha timu yake kupata ushindi wa bao 1-0.

Matokeo hayo ya kupoteza yalimaliza mbio bora za Wovles katika soka la Ulaya tangu ilipofikia hatua ya fainali ya UEFA mnamo mwaka 1972 na nafasi zake za kufuzu ligi ya mabingwa barani humo.Kwa wakati huu Sevilla walikaa kwenye mwendo wa kupanua rekodi ya mataji sita katika mashindano. Kwa upande wake Manchester United itashuka dimbani Jumapili ijayo katika mchezo wa nusu fainali.

"Tulijua tulilazimika kufanya kazi sana na ninadhani timu yangu ilicheza mchezo mzuri, hasa mchezo tuliotarajia,”kocha wa Sevilla Julen Lopetegui alisema kupitia mtafsiri. Baada ya kuokolewa kwa penaiti na kuongeza kuwa,”tuliudhibiti mchezo.”

"Nadhani goli hilo ni haki,” alisema Lopetegui.

Chanzo: AP