1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Odinga aimarisha harakati za upinzani

12 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CoaZ

NAIROBI.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya bwana Raila Odinga ametoa mwito wa kufanyika maandamano na mikutano ya hadhara nchini kote kwa muda wa siku tatu ili kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita. Bwana Odinga anapinga matokeo ya uchaguzi huo kwa sababu amesema udanganyifu ulifanyika.

Lakini polisi ya Kenya imesema itazuia maandamano hayo yanayokusudiwa kufanyika kuanzia jumatano hadi ijumaa wiki ijayo.

Hapo awali chama cha upinzani pia kilijaribu kuandaa maandamano. Lakini polisi pia ilizua harakati hizo za upinzani.

Katika hatua ya kuimarisha shinikizo dhidi ya rais Kibaki ,kiongozi wa upinzani bwana Odinga pia ametoa mwito wa vikwazo vya kimataifa na amemlaumu rais Kibaki kwa kutoonesha dhamira ya kufanya mazungumzo ya kuleta usuluhishi.

Hatahivyo katika hatua nyingine ya kujaribu kuleta upatanishi,aliekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan anatarajiwa kuanza mazungumzo mapema wiki ijayo.Wakati huio huo Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya laki tano watahitaji msaada katika wiki zijazo ikiwa mgogoro wa kisiasa nchini kenya utazidi kuwa mkubwa.