Pakistan yaondoa marufuku kwa usaifiri wa ndege za India:
30 Novemba 2003Matangazo
ISLAMABAD: Miaka miwili baada ya kusitishwa kila aina ya usafiri kati ya India na Pakistan, serikali mjini islamabad imesisitiza niya yake ya kuondoa marufuku kwa usafiri wa ndege za India katika anga zake. Mtawala wa kijeshi wa Pakistan, Pervez Musharraf alisema uamuzi wake huo utatangazwa hapo Jumatatu ya kesho yatakapoanza mazungumzo ya mapatano pamoja na India juu ya kuanzishwa tena harakati za usafiri wa ndege kati ya nchi mbili hizo. Pia huko mkoani Kashmir yameendelea kuheshimiwa yale mapatano ya kunyamazishwa silaha yaliyokubaliwa hapo Jumatano kati ya India na Pakistan.