Papa Francis aanza ziara Kongo na Sudan Kusini
31 Januari 2023Matangazo
Papa Francis hii leo anazuru mataifa hayo mawili ambayo pia yamekumbwa na umaskini, mizozo na kile Francis alichokiita mawazo ya kikoloni ambayo bado yanaichukulia Afrika kama bara lililo tayari kunyonywa. Mashirika ya misaada yanatumai ziara ya Francis itamulika mizozo iliyosahauliwa ya mataifa na kuamsha tena nadhari ya kimataifa kuhusu mizozo mibaya zaidi ya kibinadamu barani Afrika, katikati mwa uchovu wa wahisani na vipaumbele vipya vya misaada nchini Ukraine. Lakini ziara ya papa pia itamleta uso kwa macho na mustakabali wa Kanisa Katoliki, katika bara ambalo ni moja ya maeneo pekee ambako kundi la waumini wa Kanisa Katoliki linakua, katika muktadha wa ufanyaji ibada pamoja na miito mipya ya ukasisi na maisha ya kidini.