1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Papa Francis awasili kisiwa cha Corsica nchini Ufaransa

15 Desemba 2024

Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis amewasili hii leo Jumapili katika kisiwa cha Corsica nchini Ufaransa, katika ziara ya kwanza ya papa kwenye kisiwa hicho.

https://p.dw.com/p/4oAC7
Papa Francis azuru Corsica, Ufaransa
Papa Francis akiwasili katika kisiwa cha Corsica kilichopo nchini Ufaransa, Disemba 15, 2024Picha: Alessandra Tarantino/AP Photo/picture alliance

Kwenye ziara hiyo ya kwanza ya papa katika ksiwa hicho chenye idadi kubwa ya waumini wa Katoliki, kiongozi huyo atakutana na Rais Emmanuel Macron.

Papa Francis anakwenda Ufaransa, wiki moja baada ya shughuli kubwa ya kufunguliwa tena kanisa kuu la Notre Dame mjini Paris, ambayo alitangaza kutohudhuria, hatua iliyoibua mshangao mkubwa. Kanisa hilo, liliharibiwa vibaya kwa moto, miaka mitano iliyopita.

Mbali na kuzungumza na Macron, Papa Francis ataongoza ibada itakayokutanisha maelfu ya waumini wa Katoliki, akiwa ni papa wa kwanza kuzuru kisiwa hicho cha Corsica chenye idadi kubwa ya waumini kanisa hilo, miongoni mwa wakazi 350,000.

Hii itakuwa ziara yake ya mwisho ya nje ya nchi, kabla ya kurejea Rome kwa ajili ya msimu wenye shughuli nyingi wa Krismas.