MigogoroMashariki ya Kati
Papa Francis azungumzia "ukatili" unaotendeka Gaza
21 Desemba 2024Matangazo
Kwenye hotuba yake aliyotoa katika makao makuu ya kanisa katoliki duniani mjini Vatican, kiongozi huyo wa kiroho amesema kile kinachoendelea Gaza ni "ukatili na siyo vita", akizungumzia mashambulizi yanayofanywa na vikosi vya Israel kwenye ukanda huo wa Wapalestina.
Baba Mtakatifu Francis pia amezungumzia jinsi mashambulizi hayo yalivyomzuia mwakilishi wa ngazi ya juu wa kanisa katoliki kuutembelea Ukanda wa Gaza. Papa Francis amesema hapo jana Kadinali Pierbattista Pizzaballa alizuiwa kuigia ukanda wa Gaza tofauti na alivyoahidiwa.
Vita kwenye Ukanda wa Gaza vialianza Okotba 7 mwaka jana baada ya wapiganaji wa kundi la Hamas kuishambulia Israel na kusababisha vifo vya watu 1,200.