1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris: Rais Mbeki ashangilia jukumu la Chirac Kiongozi wa Afrika Kusini Thabo ...

19 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzx
Mbeki jana alishangilia juhudi za Rais Jacque Chirac wa Ufansa barani Afrika, baada ya viongozi wawili kuepuka mabishano kuhusu ombi la Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa michuano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2010. Katika hotuba yake mbele ya bunge la Ufaransa, Mbeki alimshukuru Chirac kuhusu jukumu la ulinzi wa amani la vikosi vya Ufaransa nchini Ivory Coast na kuunga mkono mradi wa maendeleo NEPAD barani Afrika. Chirac aliitisha maendeleo zaidi ya Ushirikiano mpya wa Maendeleo Barani Afrika (NEPAD), katika mkutano wa viongozi wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda G8, uliokaribishwa na Ufaransa mjini Evian na nchi wanachama ziliahidi kuharakisha hatua za kupunguzwa madeni barani humo.