Platini kuongoza UEFA kwa muhula wa tatu
23 Machi 2015Platini mwenye umri wa miaka 59, ana uhakika wa kuchaguliwa tena katika Mkutano Mkuu wa UEFA unaoendelea mjini Vienna, kwa sababu hakuna yeyote kutoka kwa mashirikisho 54 ya kitaifa aliyejitokeza kumpinga.
Baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa UEFA mwaka wa 2007, nyota huyo wa zamani wa Juventus na mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya Ballon d'Or alirejeshwa uongozini mwaka wa 2011 na tena anachaguliwa kwa mara ya tatu.
Katika uongozi wake wa miaka minane, Platini meimarisha hadhi ya Ligi ya Mabingwa, mojawapo ya tamasha maarufu zaidi na lenye thamani kubwa katika kandanda ulimwenguni. UEFA inasema dimba la mwaka huu litatazalisha euro bilioni 1.34.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman