Poland kuchukua kijiti cha Urais wa zamu wa EU mwakani
30 Desemba 2024Matangazo
Poland ni miongoni mwa nchi zilizo msitari wa mbele katika kuiunga mkono Ukraine tangu ilipovamiwa na Urusi mwaka 2022, huku Hungary ambayo ni mshirika wa karibu wa Urusi imekataa kuiunga mkono Ukraine. Mzozo wa Ukraine umekuwa ajenda kuu kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Brussels na mara kwa mara Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amejikuta akizozana na viongozi wa Umoja wa Ulaya. Kwa muda mrefu, Poland na Hungary zimekuwa na uhusiano thabiti wa kitamaduni na kidiplomasia, lakini katika miaka ya hivi karibuni nchi hizo mbili za Ulaya zimetofautiana katika maswala kadhaa na kusababisha uhusiano wao kuzorota.