1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA: Viongozi watano wa kiafrika watakutana kesho mjini Pretoria Afrika Kusini ...

26 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFxf

kuchunguza maendeleo ya muwafaka wa amani kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda. Bheki Khumalo, msemaji wa rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, alisema anataraji Mbeki atakutana na marais Joseph Kabila wa Kongo, rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Yoweri Museveni wa Uganda. Watachunguza utekelezaji muwafaka huo baina ya Kongo na Rwanda uliopatikana mjini Pretoria Julai 30 mwaka jana, na ambapo Rwanda ilikubalia kuhamisha majeshi yake Kongo kufuatia vita vya miaka mine. Wakati huo huo waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Charles Murigande ameitaka Kongo ichukue hatua dhidi ya Wahutu wenye siasa kali, ambao walikimbilia Kongo wakati wa mauwaji ya kinyama mwaka 1994.