1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRETORIA´:Afrika kusini yautua mzigo wa upatanishi nchini Ivory Coast

31 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEfu

Afrika kusini imearifu kwamba imekamilisha jukumu lake kama mpatanishi kwenye mazungumzo ya kutafuta amani nchini Ivory Coast.

Waziri wa mambo nje wa Afrika Kusini Aziz Pahad amewaambia waandishi habari mjini Pretoria kwamba jukumu la kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa liko kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Hayo yakiarifiwa hali ya wasiwasi inaendelea kuongezeka nchini Ivory Coast ambapo waasi wametishia kuususia uchaguzi mkuu wa Oktoba na badala yake wanamtaka rais Laurent Gbagbo kujiuzulu na kujitenga na siasa za mpito jambo ambalo limepingwa na chama tawala nchini humo.

Vyama vingine vya upinzani pia vimeungana kuunga mkono wito huo wa waasi wakisema uchaguzi hauwezi kufanyika kama ilivyopangwa Oktoba 30.