PSG, Benfica zapata ushindi Champions League
17 Februari 2016Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani ndio walioifungia PSG mabao wakati John Obi Mikel akiifungia Chelsea na kuipa matumaini ya kupeleka nyumbani London faida ya goli la ugenini ambalo huenda likawasaidia katika mchuano wa marudiano mnamo Machi 9. Kocha wa Chelsea Guus Hiddink amesema watajaribu kuitumia vyema faida ya goli la ugenini isipokuwa amekiri kuwa PSG ina kikosi thabiti ambacho kina uwezo mkubwa wa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali
Katika mchuano mwingine Benfica ilihitaji bao la dakika ya mwisho lililofungwa kwa njia ya kichwa na Jonas ili kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya zenit St Petersburg mjini Lisbon. Bao hilo lilifungwa katika muda wa majeruhi baada ya mchezaji wa Zenit Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano na hivyo kutimuliwa uwanjani.
Leo usiku, klabu ya Ujerumani Wolfsburg itakuwa ugenini kupambana na Gent ya Ubelgiji wakati Miamba wa Uhispania Real Madrid wakicheza ugenini Italia dhidi ya AS Roma.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Daniel Gakuba