PSG yamwadhibu mchezaji Serge Aurier
16 Februari 2016Aurier ameondolewa katika orodha ya wachezaji watakaounda kikosi kitakachopambana na Chelsea, baada ya kumtusi kocha laurent Blanc na wachezaji wenzake.
Mlinzi huyo raia wa Cote d'Ivoire atachukuliwa hatua za nidhamu baada ya kutoa matamshi ya matusi kwa kocha Laurent Blanc na wachezaji ikiwa ni pamoja na Angel Di Maria na Zlatan Ibrahimovic.
Hata hivyo Serge Aurier aliomba radhi haraka kwa kocha, wachezaji wenzake na klabu kwa jumla.
Paris St. Germain inakumbana na Chelsea katika mchezo wa kwanza wa duru ya kwanza ya mtoano kesho ikiwa ni kama mchezo wa marudio wa msimu uliopita , ambapo Chelsea ilipata ushindi mwembamba kwa wingi wa mabao. Mara hii timu zote zinaonesha hakuna atakayetaka kuondoka mapema. Nilizungumza na mwenzangu Bruce Amani kuhusu mpambano huo na mingine ya Champions League kati ya Benfica na Zenit St. Petersburg , na AS Roma ikiwa mwenyeji wa Real Madrid.
Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae /zr /
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman