1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin akutana na Jenerali anayeongoza vita Ukraine

19 Agosti 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekutana na Kamanda wa oparesheni za Urusi nchini Ukraine katika makao makuu ya jeshi kwenye mji wa Rostov-on-Don, kwa mujibu wa taarifa za Ikulu ya Kremlin.

https://p.dw.com/p/4VLiB
Russlands Präsident Wladimir Putin gibt eine Pressekonferenz in St. Petersburg
Rais Vladimir Putin wa Urusi Picha: Sergei Bobylev/TASS/imago images

Mji huo ulioko kusini mwa Urusi karibu na Ukraine, umekuwa kitovu cha oparesheni za vikosi vya Moscow nchini Ukraine.

Hata hivyo, Kremlin haikutoa maelezo ya lini mkutano huo umefanyika lakini kulingana na video zilizoonyeshwa na vyombo vya habari vya taifa, zinaashiria kwamba mazungumzo hayo yamefanyika usiku.

Mkutano huo wa Putin na Majenarali umefanyika baada ya Marekani kuidhinisha upelekwaji wa ndege za kivita chapa F-16 za Uholanzi na Denmark nchini Ukraine.

Putin ameonekana akisalimiana na mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa Urusi Valery Gerasimov ambaye hajaonekana sana hadharani tangu uasi wa kundi la Wagner ambalo lilikuwa linataka aondolewe.