Putin aomba radhi baada ya ajali ya ndege ya Azerbaijan
28 Desemba 2024Matangazo
Ikulu yake imetangaza kuwa kwenye mawasiliano ya simu baina ya viongozi hao wawili, "Vladimir Putin aliomba radhi kwa tukio hilo la kusikitisha." Putin aliripotiwa pia kuelezea kuwa katika kipindi hicho cha ajali, jeshi la ulinzi wa anga la Urusi lilikuwa likikabiliana kikamilifu na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine. Hata hivyo, hakuweka wazi kama hali hiyo ya kujilinda ndiyo iliyosababisha kushambuliwa kwa ndege. Ndege ya abiria ya shirika la Ndege la Azerbaijan, iliyokuwa inatokea Baku kuelekea Grozny, mji mkuu wa eneo la Chechnya, ilianguka siku ya Jumatano huko Kazakhstan.