Mikoa ya 4 ya mashariki Ukraine yaridhia kujiunga na Urusi
30 Septemba 2023Rais wa Urusi Vladimir Putin leo hii amesema wakaazi wa mikoa minne ya Ukraine inayodhibitiwa na serikali yake wameonesha nia yao ya kuwa sehemu ya Urusi katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa hivi karibuni.Putin ameyazungumza hayo kwa kigezo cha kura ya maoni ya mwaka uliopita, ambayo mataifa ya magharibi yaliitaja kuwa ni haramu.Katika taarifa yake iliyotolewa kwa njia ya vidio akizungumzia maadhimisho ya mwaka mmoja wa tangazo lenye utata la Urusi kuyanyakua maeneo manne ya Ukraine, Putin alisema chaguo la maeneo hayo kujiunga na Urusi limeimarishwa na uchaguzi huo wa mwezi huu uliowarejesha maafisa wanaounga mkono unyakuzi wa serikali yake.Ikumbukwe tu, Septemba 30, mwaka 2022, mikoa ya Ukraine ya Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhzhia iliingizwa rasmi katika mamlaka ya Urusi baada ya kura ya maoni ambayo serikali ya Moscow ilisema imeridhiwa na wengi.