1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PYONGYANG: korea Kaskazini kurejea kwenye meza ya mazungumzo juu ya mpango wake wa Nuklea

17 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF2c

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong- il amesema huenda ikarejea kwenye mazungumzo ya pande sita juu ya mpango wake wa Nuklea mapema mwezi ujao. Kiongozi huyo ameyasema hayo kufuatia mkutano wake na waziri wa Korea kusini anayeshughulikia suala la kuungana kwa korea zote mbili,Chung Dong Young.

Chung amemnukulu kiongozi huyo akisema kibarua kitakuwa cha Marekani kuitambua Korea Kaskazini kuwa mshirika wake.

Korea kaskazini ilijiondoa kwenye mazungumzo ya pande sita juu ya mpango wake wa silaha za Nuklea mwaka mmoja uliopita.