PYONGYANG Korea Kaskazini kurejea kwenye meza ya mazungumzo
8 Juni 2005Matangazo
Korea ya Kaskazini itarejea kwenye meza ya mazungumzo ya pande sita juu ya mpango wake wa nuklia.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imefahamisha hayo, hata hivyo Korea Kaskazini haikusema lini itarejea kwenye mazungumzo hayo.
Makubaliano hayo yaliafikiwa mjini New York katika mkutano wa pande mbili baina ya Marekani na Pyongyang.
Pande sita zinazoshiriki katika mazungumzo hayo ni pamoja na China, Japan, Korea zote mbili, Marekani na Urusi.