PYONGYANG. Korea Kaskazini yaapa kuendeleza majaribio ya makombora
6 Julai 2006Korea Kaskazini imeapa kuendeleza majaribio ya makombora yake licha ya pingamizi kubwa kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Wakati huo huo jamii hiyo ya kimataifa imeshindwa kuafikiana juu ya hatua za kuichukulia Korea kaskazini.
Korea Kaskazini katika taarifa iliyotoa imeonya kwamba itakabiliana kivitendo na nchi yoyote itakayo jaribu kupinga azimnio lake la kutekeleza majaribio zaidi.
Japan ikiungwa mkono na Marekani na Uingereza imewasilisha mapendekezo mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa yanayolenga kuwekewa vikwazo Korea Kaskazini.
Waziri wa mabo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice amesema…….O ton……nchi zote duniani zina wasi wasi juu ya uchokozi wa majaribio ya makombora yaliyofanywa na Korea kaskazini.
China imeyapinga mapendekezo hayo na badala yake imesema kuwa itampeleka mtetezi wake mkuu wa maswala ya kinyuklia wiki ijayo nchini Korea kaskazini kufanya mazungumzo na nchi hiyo.
Korea Kaskazini jana ilirusha makombora saba katika majaribio yake likiwemo kombora la masafa marefu ambalo lilianguka katika bahari ya Japan muda mfupi tu baada ya kurushwa.